EPL ARSENAL VS MAN CITY KUANZA MECHI YA KWANZA

Mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City wataanza msimu kwa mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal wikendi ya 11-12 Agosti msimu mpya wa Ligi Kuu England utakapoanza.
Arsenal wataanza msimu wakiwa na meneja mpya Unai Emery aliyemrithi Arsene Wenger, Mfaransa aliyeondoka klabu hiyo baada ya kuwa kwenye usukani kwa miaka 22.
Tottenham watasafiri Newcastle kisha wacheze dhidi ya Fulham katika uwanja wa Wembley wakisubiri uwanja wao mpya unaogharimu £850m umalize kujengwa.
Manchester United watakuwa wenyeji wa Leicester City, Liverpool nao wakutane na West Ham, huku mabingwa
wa Championship Wolverhampton Wanderers wakialika Everton uwanja wao wa Molineux.
Ninataka Arsenal wawe klabu bora zaidi duniani - Emery
Emery ateuliwa meneja mpya wa Arsenal
Fulham waliopandishwa daraja watakuwa wenyeji wa Crystal Palace, huku Cardiff wakiwazuru Bournemouth.
Chelsea watasafriHuddersfield, Southampton wawe wenyeji wa Burnley, nao Watford wakabiliane na Brighton uwanjani Vicarage Road.
Mechi za wikendi ya kwanza
Arsenal v Manchester City
Bournemouth v Cardiff City
Fulham v Crystal Palace
Huddersfield Town v Chelsea
Liverpool v West Ham United
Manchester United v Leicester City
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Southampton v Burnley
Watford v Brighton
Wolverhampton Wanderers v Everton
Mechi zitakazofuata:
JUMAMOSI 18 AGOSTI
Brighton & Hove Albion v Manchester United
Burnley v Watford
Cardiff City v Newcastle United
Chelsea v Arsenal
Crystal Palace v Liverpool
Everton v Southampton
Leicester City v Wolverhampton Wanderers
Manchester City v Huddersfield Town
Tottenham Hotspur v Fulham
West Ham United v AFC Bournemouth
JUMAMOSI 25 AGOSTI
Arsenal v West Ham United
AFC Bournemouth v Everton
Fulham v Burnley
Huddersfield Town v Cardiff City
Liverpool v Brighton & Hove Albion
Manchester United v Tottenham Hotspur
Newcastle United v Chelsea
Southampton v Leicester City
Watford v Crystal Palace
Wolverhampton Wanderers v Manchester City
LihatTutupKomentar