CHELSEA YASITISHA UKARABATI WA UWANJA WAO

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich amesitisha ukarabati wa uwanja wa klabu hiyo baada ya Visa yake ya Uingereza kucheleweshwa
Bei ya uwanja mpya wa soka wenye uwezo wa kubeba watu 60,000 wa Stamford Bridge imeongezeka hadi £1bn baada ya kucheleweshwa mbali na mgogoro unaokabili familia moja katika eneo hilo.
Abramovich yuko tayari kuwekeza katika mradi mkubwa muhimu katika taifa ambalo haruhusiwi kufanya kazi. Visa ya Uingereza ya raia huyo mwenye umri wa miaka 51 ilikwisha wiki kadhaa zilizopita.
Mnamo 2015, mabadiliko ya harakati za kuwasilisha maombi ya kupata Visa yanawataka wanaowasilisha maombi hayo kuthibitisha walivyopata utajiri wao.

Lakini inaeleweka kwamba uamuzi wa Abramovich hautakuwa na athari zozote za uendeshaji wa klabu hiyo.
Ucheleweshaji huo wa Visa mpya unajiri huku kukiwa na ongezeko la wasiwasi wa kidiplmasia kati ya London na Moscow baada ya mpelelezi mmoja wa Urusi Sergei Skripal kuuawa katika mji wa Salisbury.
Serikali ya Uingereza imekataa kutoa tamko kuhusu kesi yake. Chelsea ilitoa taarifa ikisema kuwa klabu hiyo imesimamisha ujenzi wa uwanja wa Stamford Bridge kutokana na mazingira mabaya ya uwekezaji nchini humo.
Iliongezea: Hakuna ujenzi wowote na mipango itakayoendelea.
Klabu hiyo haijatoa wakati mwafaka wa kubadili msimamo wake. Kuna mipango ya kupeleka mechi za Chelsea katika uwanja wa Wembley kwa miaka minne itakayochukua kujenga uwanja wa Stamford Bridge.
Hatahivyo hatma ya Wembley haijulikani baada ya mmiliki wa Fulham Shahid Khan kutoa kitita cha £600m kuununua uwanja huo kutoka kwa shirikisho la soka FA licha ya kuwa hatua hiyo haina athari zozote katika uamuzi wa Chelsea.
Christian Parslow ambaye aliwacha wadhfa wake kama mkurugenzi mkuu mwaka uliopita baada ya kuhudumu misimu mitatu amesema: Umekuwa mradi mgumu .Bei imepanda. Nimefikiria kwa muda mrefu kwamba ni mradi ambao hautaanza .
''Ulikuwa mradi mgumu na ghali kifedha kutimiza.Nadhani ni uamuzi mzuri kusimamisha ujenzi wake''.
LihatTutupKomentar