TAARIFA RASMI
Kampuni ya SportPesa imetangaza kuzinduliwa kwa mashindano ya SportPesa Super Cup kwa mwaka wa 2018 yatakayoshirikisha vilabu nane (8) kutoka nchi za Tanzania na Kenya ambayo yatafanyika nchini Kenya kuanzia Juni 3-10.  SportPesaSuperCup

Klabu kongwe nchini Simba na Yanga ni moja kati ya Vilabu vinne kutoka Tanzania ambavyo vinaweza vikapata nafasi ya Kwenda Uingereza kuivaa Klabu ya Everton.
Yanga, Simba, Singida United na JKU ni moja ya Vilabu kutoka Tanzania ambavyo vitashiriki Michuano maalumu ya SportPesa inayotarajia Kuchezwa mwezi ujao nchini Kenya na Bingwa wa Michuano hiyo atasafiri Uingereza Kumenyana na Everton.
Hivyo Yanga na Simba kama mmojawapo atafanikiwa kubeba Ubingwa Huo basi itakuwa ni nafasi ya Kupaa kwenda Uingereza kuivaa Everton
Msimu uliopita  Gor Mahia ndiyo waliokuwa mabingwa wa michuano hiyo na Everton walitua Nchini kucheza na Gor Mahia

LihatTutupKomentar