OKWI, ULIMWENGU LAO MOJA.

Na: MOSES FRANCIS

Emmanuel Okwi ana sifa zote za kuwa mchezaji wa kulipwa. Okwi anajitambua, ana nidhamu, na anajitunza. Kuna tatizo moja ambalo Okwi analo, si mpambanaji na mvumilivu. Watu wa karibu na benchi la ufundi la Simba wanasema Okwi hapendi sana mazoezi. Okwi kabla hajarudi simba alikuwa nchini Denmark akicheza soka la kulipwa, baadae alirudi akidai alikuwa hachezi mara kwa mara na hivyo alipoteza hali ya kujiamini. Okwi alishindwa tu kuweka mambo wazi. Iko hivi kwa wenzetu ulaya huwezi ukawa unapangwa kwenye kikosi wakati huonyeshi hali yeyote ya kuipambania namba yako ndani ya uwanja ukianzia mazoezini.
Hapo ndipo utakapoanza kupata picha kwa nini Okwi alishindwa maisha ya soka nchini Tunisia na baadae Denmark. Mshambuliaji Thomas Ulimwengu juzi alisajiliwa na klabu ya Al Hidal ya nchini Sudan. Ni taarifa ambazo zimeniumiza na zimenisikitisha.

Ulimwengu ameshindwa kuvumilia maisha ya soka barani ulaya. Mwaka jana alipata majeraha ambayo yalimweka nje kwa miezi 5. Ulimwengu alikuwa hachezi kwasababu alikuwa ametokea katika majeruhi. Leo sitaki niongee sana kwasababu Ulimwengu alikuwa anauwezo wa kupata timu hata daraja la 2 ulaya akacheza na akarudisha kiwango chake lakini si kurudi Afrika.
Kwa sasa safari imeshakuwa ngumu kwa Ulimwengu kupata timu ya daraja la juu barani ulaya. Amerudi Afrika sehemu ambayo mawakala ni wachache kupatikana. Ulimwengu anaonekana ana fuata njia ya Emmanuel Okwi ambayo amewahi kuipita. Katika timu ya taifa tutaendelea kuwa na kikosi chenye wanajeshi wachache
LihatTutupKomentar