MASTAA WA VPL WANAOWEZA KUSEPA MSIMU UJAO.


Na MOSES FRANCIS

 Kizuri chajiuza.Ni msemo wa wahenga ambao huwa una maana ya kuwa daima bidhaa au huduma  nzuri huwa inatafutwa pale ilipo. Sasa inshu iko hivi katika ligi kuu Tanzania bara maarufu kama VPL kuna mastaa kadhaa ambao wameupiga mpira mwingi balaa mpaka kufikia  hatua ya kujiuza kwa maana ya kutakiwa na vilabu vingine vikubwa baada ya kuwa wameuwasha moto uwanjani si kitoto. Makala hii inakuletea baadhi ya nyota wa VPL ambao wamecheza kwa kiwango kikubwa mpaka kuwa katika rada ya kutakiwa na vilabu vikubwa nchini Tanzania pamoja na nje ya Tanzania.

5.ALLY ALLY Beki huyu kutoka katika klabu ya stand united kutoka mkoani shinyanga anaingia katika orodha hii ya wachezaji ambao huenda tusiwaone msimu ujao katika klabu hiyo baada ya kucheza kwa kiwango cha juu ndani ya klabu hiyo maarufu kama chama la wana.Akiwa na umbo lake fupi lakini beki huyu amekuwa msumbufu kwa washambuliaji wa timu ndogo na kubwa.

4.ADAM SALAMBA Ni mshambuliaji ambaye amewahi kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa nyakati tofauti tofauti. Amekuwa ni mshanbuliaji tishio kunako katika klabu ya lipuli fc ya mkoani Iringa kwa maana ya kuwa na mwendelezo wa kuzifumania nyavu kama hana akili nzuri.Adam salamba huenda akasepa msimu ujao na kutimkia klabu kama Yanga ambayo tayari kuna tetesi kuwa imeshaanza nae maongezi.

3.MARCEL BONAVENTURE. Ndiye mshanbuliaji anayeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa wafungaji bora msimu huu akiwa nyuma ya Emmanuel okwi pamoja na John bocco. Mshambuliaji huyu kutoka katika klabu ya Maji Maji ya mkoani Iringa huenda akaihama klabu hiyo na kutimkia klabu nyingine baada ya kuwa ameonyesha kiwango kikubwa msimu huu.

2.SHAFIQ BATAMBUZE.Beki huyu raia wa uganda alisajiliwa na matajili wa alizeti kwa maana ya klabu ya singida united ya mkoani singida akitokea katika klabu ya sofapaka ya nchini kenya . Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba pamoja na kupandisha timu kunako katika klabu ya singida united huenda akahitajika kunako katika vilabu mbalimbali. Beki huyu amewahi kuichezea klabu ya simba kwa siku za nyuma.

1.EMMANUEL OKWI kasi yake ya kucheka na nyavu imekuwa haielezeki kutokana na kiwango kikubwa ambacho mshambuliaji huyu raia wa uganda amekionesha kunako katika klabu ya Simba. Okwi ndiye mfungaji bora mpaka sasa katika ligi kuu Tanzania bara baada ya kuwa amefunga magoli ishirini mpaka sasa. Uwezo wake wa kufunga magoli huenda ukawashawishi mawakala mbalimbali kutoka ndani na nje ya bara la afrika kwa maana ya kuhitaji huduma yake.
LihatTutupKomentar