DIEGO SOMEONE KUIKOSA ATLETÌCO FINAL

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone rufaa yake imetupiliwa mbali na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na sasa ataangalia mechi ya fainali ya Europa dhidi ya Marseille akiwa jukwaani may 16.
Simeone alitolewa nje na mwamuzi na kuambiwa kupanda jukwaani kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Arsenal dimba la Emirates na mechi ya pili jijini Madrid bado alitumikia adhabu ya kuangalia mechi jukwaani.

Baada ya kutinga fainali Simeone na Atletico walikata rufaa ili kocha wao aruhusiwe kurejea katika eneo lake la ufundi mechi ya fainali baadae mwezi huu jijini Lyon lakini UEFA wamekataa rufaa hiyo.
LihatTutupKomentar