MSUVA HAKAMATIKI DIFAA EL JADIDA

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana aliifungia bao la ushindi timu yake, Difaa Hassan El- Jadida ikiilaza 2-1 Raja Casablanca Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro.
Msuva alifunga bao hilo dakika ya 76 baada ya Hamid Ahadad kuifungia Difaa Hassan El Jadida bao la kusawazisha dakika ya 45, kufuatia M Iyajour kutangulia kuwafungia Raja Casablanca dakika ya 41.
Kwa ushindo huo, Difaa Hassan El- Jadida inarejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Botola Pro kwa kufikisha pointi 41 kutokana na mechi 26.
Na Msuva akapumzishwa baada ya kazi hiyo nzuri, nafasi yake ikichukuliwa na Lahoucein Khoukhouch dakika ya 87.
Japokuwa Msuva yupo katika msimu wake wa kwanza Difaa Hassan El- Jadida baada ya kununuliwa kutoka Yanga SC ya Dar es Salaam Julai mwaka jana, lakini tayari ni mchezaji tegemeo wa timu hiyo iliyofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. MSUVA AIFUNGIA DIFAA EL JADIDA BAO LA USHINDI DHIDI YA RAJA CASABLANCA

LihatTutupKomentar