Mayanga asikitishwa na Uongo huu.



Kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania taifa stars salum mayanga ameeleza kusikitishwa na uongo unaoendelea  kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa anawachukia wachezaji kutoka klabu ya yanga kwakusema anaamini mungu atamlipia kwa yeyote anayehusika kumchafua.

Akizungumza na ABM FM radio ya Dodoma kwa njia ya simu kutoka mjini mwanza mayanga amesema uzushi wote unaoenezwa juu yake kupitia mitandaoni anaufahamu ila hajui wanaomzushia wana ajenda gani dhidi yake.

Ujumbe unaodai kocha huyo kuwachukia wachezaji kutoka klabu ya yanga umekuwa ukisambazwa hasa kupitia mitandao ya wanachama wa klabu hiyo kongwe nchini.

Kwenye ujumbe huo kuna madai kuwa kocha huyo wa taifa stars amekuwa akiwatisha wachezaji wanaowindwa na yanga kuwa kama watakubali kusajiliwa na timu hiyo hatowateua tena kuchezea stars.

Akijibu tuhuma hizo kwa uchungu mayanga amesema waliozua uongo huo anaamini hawamjui vizuri na kuongeza"wakati nilipokuwa msaidizi wa mart nooij Mimi ndiye niliyemshauri tukateua wachezaji tisa kutoka yanga"amehoji mbona hakuna aliyeuliza.

Aidha mayanga amesema wakati huo kuna wanayanga walikuwa wanataka golikipa Deo Munishi aondolewe stars lakini ni yeye aliendelea kushikilia msimamo wa kubaki naye kwa sababu hapakuwa na kipa mwenye uwezo kama wake.

Juu ya malalamiko ya mashabiki wa yanga amewataka waukubali ukweli juu ya kikosi chao kwakusema"angalia centre beki alikuwa bossou,kwenye viungo kuna kamusoko na niyonzima wakati safu ya ushambuliaji ni ngoma,tambwe na chirwa"pale nifanyeje kama si kunionea?

Kocha huyo wa stars amesema atakuwa mtu wa ajabu kuacha wachezaji wanaoweza kumletea mafanikio na kuandika rekodi nzuri ambalo ndilo lengo la watanzania wote.

Amesema kwakutambua mapungufu kwenye safu ya ulinzi amekimuomba kelvin yondan aje kuimarisha nguvu.hata hivyo yondan amemuomba amuache ili akamilishe mipango ya   ndoa yake kwanza.

Aidha mayanga amesema amemtumia simon msuva ambaye amemtaja kama roho yake kwenye kikosi cha stars azungumze Geoffrey mwashiuya aongeze bidii kuinua kiwango chake kwani anamuhitaji kumjumuisha kwenye taifa stars.

Ameeleza kusikitishwa kupungua kiwango kwa juma mahadhi na Dante kwani ni wachezaji aliotegemea kuwemo kwenye stars

Kuhusu golikipa Ben kakolanya amesema bado ni kipa namba mbili wa taifa stars ila kwa sasa amempumzisha kwakuwa aliumia nyonga wakati wako mazoezini nchini afrika kusini.

Amesema hata beki wa Julia kessy ramadhan naye ameumia nyonga lakini analazimika kuwa naye kwenye kikosi kutokana na maneno haya ya uzushi yanayoendelea juu yake.

Juu ya nahodha wa zamani wa taifa stars nadir haroub amesema hawezi kumuita kwa sababu mchezaji huyo alitangaza kujiuzulu kwani hata alipoitwa na mtangulizi wake Charles mkwassa aligoma kujiunga na stars.

Hata hivyo mayanga amesema nadir,haji mwinyi,salum makapu na aggrey morris inakuwa vigumu kuwaita baada ya Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho la soka barani Africa.

Akiionyesha masikitiko juu ya tuhuma zinazielekezwa kwake amesema "hivi mayanga kweli naweza kupambana na taasisi kubwa kama yanga" ameuliza kwa mshangao.

Amesema baada ya Jana taifa stars kutoka sare ya 1-1 na Rwanda anajua kuna walioshangilia jambo ambalo amesema linahatarisha umoja wa watanzania kupitia michezo.
LihatTutupKomentar